Monday, February 5, 2018

MPENZI ASIYEKUPENDA


SURA YA SITA
DALILI 20 ZA MPENZI ASIYEKUPENDA

(1)        Haonyeshi nia ya kujali maisha yako haswa katika mambo madogo madogo kama vile kukukumbuka na kukupigia simu au kutuma ujumbe mfupi. Atajifanya yuko bize sana na hana muda wa kujenga penzi lenu.

(2)        Haonyeshi hamu ya kuboresha uhusiano wenu katika maeneo mbalimbali. Hakuna mambo mapya yanayoweza kuongezea utamu katika uhusiano wenu.

(3)        Huanzisha mzozo ugomvi bila kujali athari yake kwa uhusiano wenu kwa ujumla.Anajua vitu ambavyo huvipendi lakini bado anaendelea navyo bila kujali hisia zako. Kwa mfano anajua hupendi ukipiga simu isipokelewe lakini zaidi ya mara 2 imetokea hivyo. Asikudanganye kuwa alisahau sebuleni kwani anaekupenda atathamini mawasiliano na ni muhimu kwake atarajie kupigiwa na wewe.

(4)        Mara nyingine hukwepa kuzungumzia mambo ya sasa na kupendelea kuzungumzia mambo ya baadae kama vile kufunga ndoa au miradi mingine ya kimaisha.

(5)        Wazazi wake hawakufahamu vizuri au hakusifii kwa wazazi wake au marafiki zake.

(6)        Mara nyingi husema kuwa hana uhakika juu ya mambo ya mbele ya uhusiano wenu na kutumia lugha ya “ni mapema sana” au kusema hajui la kukuambia juu ya maisha au mwenendo wake wa baadae.

(7)        Hakuamini vya kutosha na hivyo kuonyesha wasiwasi katika maeneo mengi jambo ambalo linakukosesha raha.

(8)        Unapata shida kuongelea juu ya mambo ambayo ni ya muhimu sana kwako kwa kuwa huenda atayapuuzia au kutoonyesha ushirikiano. Hii ni moja kati ya dalili kubwa sana ya kuangalia.

(9)        Huwezi kuanzisha mazungumzo juu ya mapungufu unayoyaona katika uhusiano wenu bila ya kuanzisha ugomvi.

(10)     Anaweza kukutukana au kuonyesha dharau kwako mbele za watu na hata kama ni utani tambua kuwa anaonyesha kuwa hupendwi na huheshimiwi.

(11)     Tendo la ndoa ni kwa ajili yake pekee na hajali haja yako au kuridhika kwako katika tendo hilo.

(12)     Hayuko tayari kukufanyia mambo mazuri sawa na yale unayomfanyia wewe.ANAPENDA na kusisitiza kuwa anastahili hili na lile lakini hathamini  haja za moyo wako.

(13)     Haonyeshi kwa watu wengine kuwa kwake wewe ni muhimu na wa kipekee na hukwepa kuonekana na wewe mara kwa mara.

(14)     Mara nyingine anapenda kutoka peke yake na hahangaiki kutafuta muda wa kukaa nawe. Kama mahali mnapokuwa pamoja ni kitandani tu fahamu kuwa hakupendi hata kama anakuimbia wimbo wa NAKUPENDA kila sekunde.

(15)     Anakasirika kwa urahisi sana awapo na wewe. Uonapo anapokasirika mara kwa mara husema maneno ya dharau au kukutukana basi juwa kwamba hupendwi  bali anakuvumilia tu.

(16)     Anapata shida kuomba msamaha anapokosea kwa kuwa kwake unaonekana kuwa upo katika maisha yake kimakosa, yaani unakosea kuendeleza uhusiano wenu.

(17)     Anapata shida kuendeleza maongezi anapokuwa na wewe peke yenu.

(18)     Sio mwaminifu kwako.

(19)     Hufanya utani juu ya mambo ambayo anajua kuwa ni muhimu kwako.

(20)     Anapenda kujinunulia mwenyewe vitu vipya bila kujali kuwa na wewe ungefurahia vitu vipya na si mtoaji  mzuri wa zawadi.

2 comments:

  1. PESA/UTAJIRI WA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    MPAKA MASAA 48(SIKU 2) PAPO HAPO ULIPO KUPITIA KALAMA KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    HIZI NI DAWA NA MUDA WA UKAMILIFU WAKE NA KUKUKABIDHI

    MAJINI ZIPO AINA 3
    1. GHUUL(chma ulete)....Siku 5
    2.SAIFRAHAN(Jini wa kufuga)...Siku 6 n.k
    3.SAIFRAHA(jini wa bahati)....masaa 24

    NDAGU ZIPO AINA 6
    1.MTU.....week 1 na nusu
    2.MIMBA....siku 5
    3.UTASA....masaa 72(siku tatu)
    4.ULEMAVU....siku tano
    5.NDUGU WATATU...siku sita
    6.WANYAMA.....masaa 48

    KARIBU UPATE UFAFANUZI UCHAGUE UIPENDAYO KILA MOJA NA MASHARTI YAKE.

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    HACHA KUTANGATANGA PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI

    NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI NA KUTUNZA SIRI......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    PIGA SIMU/Whatsup +255 742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA SIMU KUEPUKA MATAPELI

    ReplyDelete