Monday, February 5, 2018

DALILI ZA MPENZI ALIEBOREKA NA WEWE

DALILI ZA MPENZI ALIEBOREKA NA WEWE

Mahusiano mengi sana yapo katika hali ya kusikitisha, na wengi hawajui wamefikaje fikaje katika hali hiyo jambo ambalo linatisha. Unapokutana na hali ambayo hujui jinsi ya kuiondoa, inatisha sana na ni sawa sawa na mtu ambae ameanguka kwenye dimbwi refu la kuogelea wakati huo na yeye hajui kabisa kuogelea. Jambo la ajabu katika mahusiano mengi ya kimapenzi ni kwamba mtu anaweza kuwa ameboreka na mpenzi wake lakini hajui afanye nini kubadili hali hiyo mbaya, na mbaya zaidi akashindwa hata kutafuta njia za kuibadili hali hiyo. Ukijua kuwa mpenzi wako ameboreka unaweza kuanza kutafuta njia za kumsaidia achangamke lakini usipojua hilo na ukaendelea kama vile hakuna tatizo unakaribisha majanga katika uhusiano wenu.Matokeo  hayo nayaona pale  mteja anaponiambia kuwa mpenzi wake kabadilika na sababu haijui    na anaumia kwa  kuwa anampenda sana.

Unapohisi kuwa mpenzi wako ameboreka upo uwezekano  mkubwa kuwa ni kweli ameboreka na haijalishi kama kosa ni lako au la kwake au mchanganyiko wa yote ya kwako au yak wake hiyo ni hali ambayo inahitaji ufumbuzi haraka.
Zifuatazo ni dalili kuwa mpenzi wako ameboreka na wewe au na uhusiano wenu kwa ujumla:


1)            Pamoja na bidii yako kubwa bado mpenzi wako anaonekana kama akili yake ipo sehemu nyingine  ofauti kabisa. Katika mazingira kama haya ndio  unasikia mtu unasema “Mpenzi wangu simuelewi” unampigia simu hapokei kwa wakati na anachelewa sana kukupigia. Unamtumia SMS nzuri za kimahaba lakini yeye anajibu kikavukavu tu, ukiuliza kitu basi anatoa majibu mafupi mafupi au mkato mkato.
2)             Mara nyingi anakuwa mzito kukujulisha nyendo zake au mizunguko yake na pindi ukihoji  juu ya mwenendo wake anakuwa mkali.

3)             Ameanza kukulinganisha na wanawake au wanaume wengine bila kujali hisia zako.

4)             Hapendelei kukuita kwa majina ya kimahaba kama baby, honey, mpenzi n.k. Pia hapendelei muongelee juu ya kiwango cha penzi na ubora wake.

5)             Unapokuwa na jambo linalo kuhuzunisha au kukukosesha raha haangaiki kukufariji. Huzuni yako au maumivu yako hayasumbui nafsi yake.

6)             Uso wake hauonyeshi uchangamfu kama pale mwanzoni. Uonapo mpenzi wako anapokuwa na wewe uso wake upo kama vile amesikia mtu alietoa hewa mbaya, tambua kuwa ameboreka na wewe kwa kiasi kikubwa.

7)             Uonapo anakasirika sana kwa mambo madogo madogo na hali hiyo ikawa inajirudia rudia hiyo ni ishara kuwa amekuchoka. Na iwapo mara kadhaa katika mazingira kama hayo anasema mambo yanayoonyesha kuachana na wewe hiyo  ni haja ya moyo wake basi tambua kuwa yasipotokea mabadiliko kifo cha uhusiano wenu hakiko mbali. Mara nyingi hali hiyo huambatana na maneno yanayokatisha tamaa.

8)  Anakwepa mada zinazohusu madhaifu au mapungufu yake. Uonapo kuwa mpenzi wako hapendi mzungumzie kwa kina mambo yanayoharibu ubora wa uhusiano wenu maana yake haoni sababu yoyote ya kupoteza muda wake katika kujenga uhusiano wenu, yaani ameishiwa nguvu za kujenga na kupamba uhusiano wenu.

9)  Mpenzi wako anapendelea zaidi kuchati na marafiki zake kuliko kuongea na wewe muwapo pamoja. Lingine linalofanana na hilo unakuta mpenzi wako anapendelea zaidi kuangalia TV kuliko kuongea na wewe muwapo pamoja. Hali hii ikiendelea mtajikuta mnaishi kama vile ni kaka na dada yake.


10) Ameanza kutumia maneno makalimakali pale unaposema bila kujali hisia zako au amekuwa mtu wa kufoka foka na kuguna guna.

11)  Uvaaji wake unakuwa wa hovyo hovyo na hajali sana kupendeza katika uvaaji wake. Ukiwa na mpenzi kama huyo na ghafla ukaona ameanza kuvaa vizuri maana yake amepata mchepuko.

12) Ni mara chache sana mmetoka pamoja kwa chakula au vinywaji au hapendi muonekane pamoja.

13) Husikilizwi kikamilifu; Ni kweli hakuna mtu anaependelea hali ya kubishana bishana lakini kuna wakati hali hiyo inajitokeza na jinsi mpenzi wako anavyo kabiliana na hali hiyo itakupa picha ya mtu alieboreka na wewe na hategemei faida yoyote ya majadiliano ya aina yoyote. Pale mpenzi wako anapoanza kukatisha mazungumzo yenu kwa kusema “Yaishe” au “Kila siku jambo lile lile tu” au “Sitaki kelele zako” tambua kuwa umekuwa kero kwake japo hoja yako ni halali kabisa. Kama vile hakuna mtu ambae anapendelea kula chakula kilichopikwa lakini hakikuiva hakuna mtu anaefurahia kuona haja yake ya kutoa yote yaliomo moyoni imekatishwa kwa sababu zisizo halali. Mpenzi anaekupenda atakusikiliza kilio chako bila kujali ni marudio kwa kuwa anaheshimu hisia zako.

14) Kaacha mambo yanayokusisimua; Mtu alie boreka na wewe utamuona ameacha kukupa surprise za hapa na pale na amekuwa mwepesi wa kuahirisha mambo mliokubaliana.


15)UCHEZAJI  wa ngoma  ya wakubwa umeanza kupungua; Chakula ambacho kimeanza kuchacha kinagundulika kutokana na kubadilika kwa ladha yake jambo ambalo linakuondolea hamu ya kula chakula hicho. Uonapo mpenzi wako amepunguza bidii yake katika kuhakikisha unaridhika na tendo la ndoa tambua ngoma hiyo imechcha na ameanza kuboreka katika eneo hilo na pia uonapo analeta visingizio vyenye ulemavu ili kuepuka kucheza na wewe ngoma ya wakubwa ni dalili ya hatari sana..

Ndugu yangu,usijidanganye kwa kusema mapenzi ndivyo yalivyo wakati  huna raha na uhusiano uliomo. UPO  uwezekano wa kuleta mabadiliko mazuri kama vile wahenga walivyosema  penye nia pana njia.Tafuta njia ya kumsaidia mpenzi wako aelewe umuhimu wa kufurahiana katika uhusiano uliomo kinyume na hapo utaishi kama mtumwa kwani hisia zako haziheshemiwi.


1 comment:

  1. PESA/UTAJIRI WA NDAGU AU MAJINI KWA MUDA MFUPI

    MPAKA MASAA 48(SIKU 2) PAPO HAPO ULIPO KUPITIA KALAMA KWA MASHARTI MAALUM KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI YA KUTUNZA SIRI HII SIO MZAHA......

    HIZI NI DAWA NA MUDA WA UKAMILIFU WAKE NA KUKUKABIDHI

    MAJINI ZIPO AINA 3
    1. GHUUL(chma ulete)....Siku 5
    2.SAIFRAHAN(Jini wa kufuga)...Siku 6 n.k
    3.SAIFRAHA(jini wa bahati)....masaa 24

    NDAGU ZIPO AINA 6
    1.MTU.....week 1 na nusu
    2.MIMBA....siku 5
    3.UTASA....masaa 72(siku tatu)
    4.ULEMAVU....siku tano
    5.NDUGU WATATU...siku sita
    6.WANYAMA.....masaa 48

    KARIBU UPATE UFAFANUZI UCHAGUE UIPENDAYO KILA MOJA NA MASHARTI YAKE.

    KUMBUKA MALIPO NI BAADA YA KUFANIKIWA

    kwa maelezo kamili piga namba +255742162843

    HACHA KUTANGATANGA PUUZA UONGOFU WA KUWA MTU KUWA TAJIRI NI DHAMBI WAKATI AKUAMBIAE YEYE NI TAJIRI

    NDANI YA MASAA 72(SIKU TATU) PAPO HAPO KIKUBWA UWE MWAMINIFU, JASILI NA UWE NA UTAYARI WA KUPOKEA MASHARTI NA KUTUNZA SIRI......

    NAITWA DR, MDIRO piga 0742162843. KAMA UNAITAJI PESA ZA MAJINI AU NDAGU YA MALI AU ULINZI KWA MALI YAKO
    (HUSITUME SMS PIGA SIMU KUHEPUKA MATAPELI)
    MATIBABU MENGINEYO NI KAMA UTULIVU KATIKA NDOA, AU KUMVUTA UMPENDAE, KUONDOA MIKOSI, MABALAA, KUOSHA NYOTA, KUITAMBUA NYOTA YAKO NA ASILI YA KAZI YAKE, KAMA UNASUMBULIWA NA MAJINI MAHABA NA SHIDA YA UZAZI.

    PIGA SIMU/Whatsup +255 742162843. KIKUBWA NI KUSIKILIZA NA KUFATA MASHARTI. ANGALIZO USITUME SMS PIGA SIMU KUEPUKA MATAPELI

    ReplyDelete